Saturday, August 10, 2013

Muhtasari wa yaliyojadiliwa katika kikao cha Tarehe 27 July 2013

Katika hatua hii wajumbe walichukua mda mrefu kujadili kwa kina mambo mapya waliokuja nao mwezi huu, hii yote na katika kuona kikundi chetu kinaandaliwa ili kiweze kujengeka vizuri na kwa uimara zaidi.

Wajumbe walijadili suala zima la kusaidiana kwa wajumbe waliopo ndani ya kikundi. Hii ni 
pamoja na kusaidiana katika MISIBA, SHEREHE(harusi na send off), MIKOPO.
Ili jambo hili liweze kutimizwa, wajumbe waliona nI vyema kutengeneza FIGURE ambayo 
itakua inaonesha mjumbe asaidiwe vipi unapotokea MSIBA, SHEREHE au MKOPO. Wajumbe  walilijadili suala hili kwa undani zaidi, wakiangalia pia mfuko wa kikundi ukoje kwa wakati huu.

Kwenye kipengele cha MSIBA wajumbe walionani vyema kutenga makundi ambayo kama 
mjumbe atapata msiba ijulikane atasaidiwa vipi. Kwanza kabisa kama mjumbe atafiwa na 
WAZAZI(baba au mama),  MLEZI,  MTOTO,  MWENZA WAKE, kikundi kitato kiasi cha shilingi laki  moja na nusu(150000).  Kama mjumbe atafiwa na MDOGO WAKE au  MKUBWA WAKE(kaka au dada),  kikundi kitatoa shilingi elfu hamsini (50,000),  wajumbe pia walijadili na kuona kama  mjumbe atapata msiba wa ndugu wengine basi kikundi kitaona ni jinsi gani kitatoa msaada.

N.B; -kwenye suala hili la msiba, pindi mjumbe anapotoa taarifa ya msiba kwa wajumbe 
wenzake, itabidi kuwepo na mwakilishi ambae ataenda msibani kuwakilisha kikundi, hii ikiwa ni pamoja na kukabidhi mchango uliotolewa na kikundi.
        -Wajumbe pia walijadili suala hili kwa kuangalia, ni msaada kiasi gani utatakiwa pindi 
mjumbe anapopatwa na msiba kulingana na hali halisi au hali ya maisha mjumbe aliyonayo. Mana fedha pekee inaeza isitoshe bali na nguvu za wajumbe zitaitajika ili kumsaidia mjumbe  atakepatwa na tatizo hilo. 

Tukija katika SHEREHE hiyo ikiwa HARUSI na SEND OFF; wajumbe waliona ni kugawanya  kipengele hiki kwenye makundi mawili; harusi kwa wavulana na send off kwa wasichana.  Kiwango kilichojadiliwa apa ni kiasi cha shilingi laki moja na nusu(150,000), yani laki moja  anapewa muhusika wa shughuli na elfu hamsini kununuliwa zawadi yenye gharama ya elfu  hamsini na kukabidhiwa muhusika siku ya sherehe. 

N.B; Kwenye suala la MSIBA na SHEREHE kiwango kinaweza kuongezwa kutokan na kiwango  chetu kwa mda ule lakini wajumbe waliona kiwango hicho kinafaa kutokana na mfuko wa  kikundi  ulivyo kwa sasa.

Kwenye MKOPO, ingawa wajumbe hawakufikia muafaka kwenye jambo hili lakini kuna machache yaliyojadiliwa.
  • Wajumbe waliona ili mjumbe aweze kukopa ndani ya kikundi ni lazima kuwepo na FORMya makubaliano ambayo itamwezesha mjumbe anaetaka kukopa kuweza kueka SAHIHI kama uthibitisho wa mkopo.
  • Pia kuwepo na kiwango ambacho kikundi kitapanga kwa ajili ya kukopesha wajumbe wake. 

Kipimo cha kukopesha ni muhimu kizingatiwe kulingana na mfuko wa kikundi ulivyo. Kisizidi kiwango kilichopo kwenye mfuko wa kikundi.
  • Wajumbe walionelea masharti ya mjumbe kukopa yasiwe magumu sana ivyo kuwafanya wajumbe washindwe kukopa, masharti yanatakiwa kuwa nafuu.
  • Sehemu yoyote ile mtu akikopa lazima kuwepo na RIBA, hivyo wajumbe waliona ni vyema na kikundi chetu kuwa na RIBA pindi mjumbe achukuapo MKOPO.

N.B;- Wajumbe waliona kwa kuwa bado hatujajua kikundi chetu haswa tuko wangapi au 
wangapi wanachukulia kwa umakini jambo hili, waliona kipengele hiki cha MKOPO kiachwe kwanza mpaka pindi itakapojulikana kikundi chetu kina wajumbe wangapi(uhakikisho huu wa jumla ya wajumbe itakua kuanzia mwezi wa tisa).
   -Pindi tutakapojulikana kisheria kwenye mfuko wa SACCOS,wajumbe watapata faida zaidi ya kupata mikopo, kupitia kikundi chetu.

Wajumbe walizidi kutilia mkazo suala la ufunguaji wa KAMPUNI, hii ni kutokana na kwamba tutakapofanikiwa kufungua kampuni kwanza TUTATAMBULIKA,  TUTAPATA TENDA MBALIMBALI mfano; usambazaji wa vitabu, mchanga, ununuzi wa mafuta.  Hii itatuezesha kufanya kazi UNDER DEBTS. Hivyo wajumbe waliona nivyema kuanza na BUSSINESS NAME tunapofungua kampuni.

Uwekezaji katika KILIMO nalo lilitiliwa mkazo  na mifano mbalimbali kutolewa, ukiwepo mfano huu wa kilimo cha UYOGA, ambapo mjumbe aliekua na taarifa japo kidogo aliweza kutoa maelezo kwa ufui kwa wajumbe wengne. Uyoga ni zao linalochukua siku ishirini na moja(21) kukua. Kuna uyoga MBICHI na MKAVU. Kinachotakiwa zaidi kwenye zao hili ni kujua MBEGU iliyobora pamoja na UDONGO. PIPI moja ya uyoga inapatikana kwa shilingi elfu moja(1000), KILO moja ya uyoga ni shilingi elfu nne(4000), kwa mtaj mdogo wa Tsh laki tatu, unapata pipi(udongo na mbegu)200, kwa pipi unaweza pata kg 8, hivyo basi pipi 200 mara kilo 8 mara 4000 unapata faida ya 6,400,000millioni.

N.B;-
  • kuanza biashara hiyokwa mtaji mdogo ni laki tatu(300,000)
  •         -kujifunza kilimo cha UYOGA ni shilingi elfu ishirini(20,000).

1 comment:

  1. Kwenye kipengele kinachohusu SHEREHE kumbukeni pia matukio ya USHEMASI NA UPADRISHO.

    ReplyDelete